Serikali imezindua rasmi zoezi la dharura la ukaguzi na usajili wa wadau wa maziwa nchini, hatua inayolenga kuongeza mchango wa sekta hiyo katika pato la taifa kutoka asilimia 2 ya sasa hadi kufikia angalau asilimia 2.3.
Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania, Profesa George Msalya, amesema sekta ya maziwa inanufaisha zaidi ya kaya milioni 4.6 nchini, hivyo kuwekwa kwenye mfumo rasmi wa mnyororo wa thamani kutasaidia kuongeza tija, ajira na mapato ya wadau.
Kwa upande wake, Afisa Mifugo wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mariam Kingu, amesema zoezi hilo ni la lazima kisheria na linakusudia kuwatambua rasmi wadau wote ili waweze kunufaika na fursa za serikali pamoja na huduma za maendeleo ya sekta hiyo.
