
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene amesema baadhi ya waajiri wanachangia watumishi wa umma kuchelewa kupandishwa vyeo kwa kutopeleka taarifa za watumishi wao kwenye wizara na kuomba kufanyiwa kazi.
Waziri Simbachawene ameyasema hayo leo bungeni jijini Dodoma akijibu swali la Mbunge wa Newala Vijijini, Maimuna Mtanda aliyetaka kufahamu kwanini baadhi ya watumishi wamechelewa kupandishwa vyeo licha ya kuwa na sifa na vigezo vya kupandishwa vyeo
Kutokana na hali hiyo amewataka waajiri wa watumishi wa umma nchi nzima kuwasilisha taarifa za watumishi wao wote wanaotakiwa kupandishwa vyeo ili zoezi hilo liweze kufanyiwa kazi kwa wakati.