
Siku chache baada ya ziara ya Waziri wa Maji Jumaa Aweso nchini China ambapo alitembelea pia Mji wa Shangai katika kiwanda cha KSB Shangai Pump kinachojihusisha na kutengeneza pampu kubwa za maji. Sasa Tanzania imeamua kuzinunua ili kuboresha mitambo ya Ruvu juu na Ruvu chini na kuondoa za zamani ambazo ufanisi wake umeshuka na zimekua na matengenezo ya mara kwa mara yanayosababisha kukosekana maji ya uhakika Jijini Dar es salaam.
Akizungumza mara baada ya ziara hiyo Waziri wa Maji Jumaa Aweso anasema Gharama za pampu hizi ni shilingi Bilioni 16.5 pamoja na ufungaji huku fedha zote hizo zikitolewa na Serikali ya Tanzania na kazi ya ufungaji ikitarajiwa kukamilika Juni 2026 ambapo ununuzi wake ni hatua za makusudi na jitihada za serikali kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji kwa Wananchi wa Dar es salaam na Pwani kupitia Wizara ya maji.
Lengo la ziara ya Timu ya Wizara ya Maji na DAWASA katika ziara hiyo ya China ilikuwa ni kushuhudia majaribio ya mwisho ya awamu ya pili ya pampu hizo ambapo Waziri Aweso amejiridhisha na aina zake, viwango na uwezo wake na kuruhusu mzigo usafirishwe kuletwa Tanzania mara moja baada ya matengenezo yake kukamilika.
Aidha, awamu ya kwanza yenye jumla ya pampu nne ilishakamilika na tayari zimeshafikishwa Dar es salaam na tayari kazi ya ufungaji imeanza na inaendelea ambapo baada ya kuwasili kwa hizo nyingine kazi itakamilishwa na zitawashwa kwa
