
Wamiliki wa shule binafsi wilayani Chato mkoani Geita wametakiwa kuhakikisha shule hizo zinakua na miundombinu rafiki ya kujifunzia kwa ajili ya watoto wenye ulemavu.
Mdhibiti mkuu wa ubora wa elimu wilayani humo Pendo Magessa amesema ni kosa kisheria kwa mmiliki yeyote wa shule kuendesha mafunzo kwa wanafunzi wenye ulemavu wakati hana miundombinu rafiki kwa ajili ya watoto hao.
Amesema kwa kuzingatia miongozo ya wizara ya elimu shule yeyote itakayobainika kutoa mafunzo kwa watoto wenye mahitaji maalumu wakati haina miundombinu rafiki kwa ajili yao itafungiwa na wahusika kuchukuliwa hatua za kisheria.
Baadhi ya wamiliki wa shule binafsi wilayani humo Esta Benjamin pamoja na Mlekwa Charles, wamesema tayari wameisha pokea mwongozo wa namna ya kuendesha mafunzo kwa watoto wenye mahitaji maalumu na kuahidi kuzingatia maelekezo hayo ili kustawisha elimu katika kundi hilo.