
Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema maendeleo ya taifa hayawezi kupatikana bila wananchi na taasisi mbalimbali kushiriki kikamilifu katika kulipa kodi kwa hiari na kwa wakati.
Dkt. Mwigulu amesema hayo June 12bungeni jijini Dodoma, wakati akiwasilisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2025/2026 na kubainisha kuwa jumla ya shilingi trilioni 56.49 zinatarajiwa kukusanywa katika mwaka huo wa fedha.
Aidha amesisitiza kuwa mapato ya ndani ndiyo tegemeo kubwa la Serikali katika kugharamia huduma za kijamii kama afya, elimu, miundombinu na usalama wa nchi na kwamba kila mmoja ana jukumu la kuhakikisha anatimiza wajibu wake wa kizalendo kwa kulipa kodi stahiki.
Ameongeza kuwa mafanikio yaliyopatikana katika ukusanyaji wa mapato ya ndani ni ushahidi kuwa Watanzania wengi wameanza kuelewa umuhimu wa kulipa kodi.
Hata hivyo, amesisitiza kuwa bado kunahitajika juhudi zaidi za kuelimisha na kuhamasisha walipakodi walioko nje ya