
Na, Jerome Robert
Dar Es Salaam
Tanzania imechaguliwa kuwa mwenyeji wa tuzo za kimataifa za utalii ‘World Travel’ na hafla ya kutangaza washindi wa Kanda ya Afrika na Bahari ya Hindi itakayofanyika Juni 28, Dar es Salaam chini ya uratibu wa Bodi ya Utalii Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii, Ephraim Mafuru amesema tuzo hizo zilianzishwa mwaka 1993 na Kampuni ya World Luxury Media Group kwa lengo la kutambua, kuthamini na kusherehekea mchango wa wadau katika sekta ya Utalii na Ukarimu duniani.
Amesema wadau wanaotambuliwa ni mashirika ya ndege, watoa huduma za malazi, vivutio vya utalii, wakala wa biashara za utalii, vivutio vya utalii, mamlaka za usimamizi na utangazaji wa utalii na wadau wengine.
Tuzo hizi zimekuwa chachu ya ubunifu, ushindani na kuboresha viwango vya huduma ya utalii kitaifa na kimataifa.
CHANZO: ITV