
Na, Jerome Robert
Dar Es Salaam
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amesema Tanzania itaendelea kushiriki na kutimiza matakwa ya kimataifa katika kupambana na kudhibiti uhalifu wa kifedha.
Majaliwa ametoa kauli hiyo leo, wakati wa ufunguzi wa mkutano kati ya ujumbe wa Tanzania na Kikosi Kazi cha Kimataifa cha Kudhibiti Fedha Haramu (FATF), uliofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania, jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa kufuatia tathmini zilizofanywa na taasisi za kudhibiti uhalifu wa kifedha Kusini mwa Afrika mwaka 2021, pamoja na tathmini ya kimataifa ya mwaka 2022, Tanzania imeimarisha mifumo ya kupambana na fedha haramu.
Majaliwa amesema kuwa hatua zilizochukuliwa ni pamoja na kujenga uwezo wa rasilimali watu, kuboresha vifaa, na kuimarisha taasisi zinazohusika na mapambano hayo.
CHANZO: TBC