
Shirika la Tanzania wote Equality Alliance (TAWEA) limezindua mradi wa utunzaji wa Mazingira katika vijiji vinne vya halmashauri ya Kasulu vijijini Mkoani Kigoma ili kutoa elimu kwa wananchi kuacha uharibifu wa hifadhi ya msitu wa Makere kusini pamoja na Pori la Akiba la Moyowosi.
Misitu ni Banuai muhimu katika uhifadhi wa Cabon ambayo inasaidia kupunguza hewa ukaa ili kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia nchi ikiwemo ongezeko la joto kote Duniani.
Katika uzinduzi wa mradi huo wa utunzaji wa Mazingira Mratibu wa mradi kutoka Shirika la TAWEA Batro Ngilangwa amebainisha kuwa zipo shughuli zitakazotekelezwa zenye lengo la kuinua na kukuza uchumi wa wananchi katika vijiji vinne vya Muvinza, Kagera nkanda, Chekenya na Kabula nzwili ambako mradi huo utatekelezwa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la TAWEA Fisto mlina ameeleza kuwa shirika hilo ambalo linatekeleza majukumu yake katika mikoa ya kigoma na Geita wanayomatumaini kuwa msitu wa Makere kusini na pori la akiba la Moyowosi ambalo kwa sehemu lipo katika wilaya ya Kibondo.
Aidha imeelezwa kuwa matarajio makubwa ni kwamba misitu hiyo irejee katika uhalisia wake baada ya kuharibiwa na binadamu kutokana na shughuli za Kilimo cha Kuhama hama.
Afisa Misitu halmashauri ya Kasulu Vijijini Bw. Hassan Omary amesisitiza kuwa ushirikishwaji wa wananchi na viongozi wa serikali ni jambo muhimu na litasaidia kupatikana kwa ushirikiano katima maeneo yote ambayo mradi huo utatekelezwa.
Ikiwa wadau hao watashirikiana kwa ukaribu zaidi na serikali inatazamiwa watafikia mafanikio ya moja kwa moja katika utekelezaji wa mradi huo hatua ambayo ameieleza Bw Almachos Josephu Njungani Afisa maendeo maendeleo ya jamii msajili msaidizi wa Mashirika ya Siyokuwa ya Kiserikali halmashauri ya kasulu Vijijini kuwa ni kuongeza kipato kwa wananchi watakao nufaika na mradi huo.