
Baraza la Maaskofu Kanisa Katoliki Tanzania TEC limelitaka Jeshi la Polisi na Vyombo vingine vya usalama nchini, kufanya uchunguzi wa haraka kubaini waliohusika na Uvamizi dhidi ya Katibu mkuu wa Baraza hilo Padre Charles Kitima, Usiku wa Kuamkia Mei Mosi Mwaka huu.
Tamko hilo limetolewa na Baraza la Maaskofu kupitia Makamu wa Raisi wa Baraza hilo Askofu Eusebius Nzigilwa Leo Jijini Dares Salaam ambapo amesema kuwa Polisi na Vyombo vingine vya usalama, vinapaswa kuwasaka na kuwakamata waliopanga tukio hilo na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria
Baraza hilo limetaka hatua za haraka za uchunguzi wa tukio hilo kufanyika na kuweka wazi taarifa zote bila kupotosha ukweli wa tukio ili kurudisha amani na matumaini kwa waumini na jamii kwa ujumla
Baraza limeendelea kuishukuru serikali, vyama vya siasa, viongozi wa dini, taasisi za ndani na za kimataifa kwa kuendelea kulaani tukio hilo na kuwataka waumini kuwa watulivu na kumuombea padre Charles kitima.
Padre Charles Kitima amevamiwa na kujeruhiwa usiku wa kuamkia leo Mei Mosi kwenye makazi na makao makuu ya baraza hilo yaliyopo Kurasini Jijini Dares Salaam na anaendelea na matibabu katika hospitali ya Agha Khan Jijini humo.