Rais wa Marekani, Donald Trump, ameiponda show ya mapumziko (halftime show) kwenye Super Bowl iliyofanywa na mwanamuziki wa Puerto Rico, Bad Bunny, akielezea kuwa “mbaya sana” na mojawapo ya maonyesho mabaya zaidi kuwahi kutokea katika historia ya tukio hilo.
Katika kauli aliyoweka kwenye Truth Social, Trump alisema onyesho hilo halikuwakilisha kile alichokitaja kuwa viwango vya Marekani vya mafanikio, ubunifu na ubora.
Trump pia amekosoa mitindo ya kucheza, akisema kuwa ilikuwa ya kuchukiza, hasa ikizingatiwa kuwa watoto walikuwa miongoni mwa mamilioni ya watazamaji waliokuwa wakitazama nchini Marekani na sehemu mbalimbali duniani.
Aidha, alitabiri kuwa onyesho hilo lingesifiwa na vyombo vya habari alivyoviita “fake news media,” akivishutumu kwa kutofahamu kinachoendelea katika dunia halisi.
Katika kauli hiyo hiyo, Trump pia aliikosoa NFL kwa kanuni yake mpya ya kickoff, akitaka ibadilishwe mara moja. Pia kupitia ukurasa wa Instagramu wa Chris Brown aliandika maneno yaliyoashiria kuibeza sho hiyo akisema , ‘Nadhani ni salama kusema kuwa wananihitaji.’
