Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, amemtaka Meneja wa TANROADS mkoa wa Mwanza, kumsimamia mkandarasi anayejenga Daraja la Mkuyuni na kuhakikisha mradi huo unakamilika ifikapo Januari 15 ,2026.
Ulega ametoa agizo hilo wakati wa ziara yake ya kikazi jijini Mwanza, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Waziri Mkuu wa Tanzania Dkt Mwigulu Lameck Nchemba ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali kuona na kufanya tahimini ya maendeleo ya miradi.
Katika ziara hiyo, Waziri Ulega ametembelea ujenzi wa Daraja la Mkuyuni, mradi ambao umefikia asilimia 75 ya utekelezaji, licha ya mradi huo kuchelewa karibu asilimia 14 ya muda uliopangwa kukamilika.
Waziri Ulega ameonesha kutoridhishwa na kasi ya ujenzi na amemuagiza mkandarasi kuongeza nguvu na rasilimali kuhakikisha daraja hilo linakamilika ifikapo Januari 15 mwakani.