Mwamuzi Kassim Mpanga Kassim Mpanga kutoka Dar-es-salaam ambaye alikuwa mwamuzi msaidizi namba moja (1) katika mchezo wa Yanga vs Simba march 1 2026 new Aman Complex amefungiwa kuchezesha kwa miezi sita (6) baada ya kukataa goli la Simba kuoitia Selemani Mwalimu katika mchezo huo.
Kassim Mpanga aliinua kibendera chake mara baada ya goli hilo kufungwa dakika ya sabini (70), akiashiria kulikua na kosa la kuotea kwa mchezaji Selemani Mwalimu kitendo kilichobainika kuwa hakikuwa cha kweli baada ya kamati kupitia tukio hilo.

Hamdan Said kutoka Mtwara amefunguwa kuchezesha boli kwa miezi mitatu (3) baada ya kuonesha kibendera dakika ya 61 ya mchezo akiashiria mchezaji wa Yanga Prince Dube ameotea pindi alipopata nafasi ya kwenda kufunga.
Adhabu hizi ni kwa mujibu wa kanuni namba 42:1(1-8) ya ligi kuu kuhusu udhibiti wa waamuzi, kanuni ambayo ilikaziwa na kauli ya rais wa TFF Wallace Karia mwanzoni mwa ligi kuu soka bara kuwa mwamuzi atakayeharibu mchezo atakutana na adhabu kali.
