
Na Asma Ahmed- Ngara
Waandishi wa habari wilayani Ngara mkoani Kagera wametakiwa kuwa msitari wa mbele katika kukemea na kuripoti vitendo vya rushwa kuelekea uchaguzi mkuuu mwaka huu 2025.
Rai hiyo imetolewa na mkuu wa Taasisi ya kupambana na Rushwa TAKUKURU Bw Ally Mickydady wakati wa warsha iliyowakutanisha viongozi wa taasisi hiyo na waandishi wa habari wa wilaya hiyo kujadili kwa pamoja namna bora ya kuzuia vitendo vya rushwa kuelekea uchaguzi huo.
Amesema kuna baadhi ya waandishi wa habari ambao wamekuwa wakinunuliwa na baadhi ya na kusababisha kuandika habari ambazo zimeeegemea upande mmoja na kwamba kufanya hivyo ni kosa kisheria .
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mafunzo hayo wamesema hawako tayari kuwa sehemu ya kuchochea vitendo vya rushwa bali watajikita kuelimisha jamii juu ya madhara ya rushwa hasa katika kipindi cha uchaguzi mkuu wa mwaka huu