
Na, Zawadi Bashemela
MBOZI
Vijana waliohitimu mafunzo ya awali ya kijeshi ya oparesheni miaka 60 ya muungano kikosi cha jeshi 845 Itaka kilichopo wilayani Mbozi mkoani Songwe wametakiwa kutumia elimu na mafunzo waliyoyapata kutatua changamoto za kijamii katika maeneo yao.
Akizungumza na vijana hao wapatao 592 mwakilishi wa mkuu wa jeshi la kujenga taifa, Kanali Amos Mollo amesema vijana hao wana jukumu la kuyatumia mafunzo hayo katika kuleta matokeo chanya katika jamii ikiwemo kutatua changamoto na kufikia lengo la Serikali.
Aidha amewaasa Vijana hao nidhamu ikawe ndio silahaa pekee dhidi ya jambo lololote litakalokuwa mbele yao, na kwamba Jeshi la kujenga taifa linanendelea kuamini kuwa kiapo cha utii walichokiapa mbele ya mgeni rasmi ni ishara tosha kuwa taifa limewekeza sehemu sahihi na litaendelea kuwa salama wakati wote.