Wizara ya afya kwa kushirikiana na kampuni ya Buffalo Bicycles Tanzania imetoa msaada wa baiskeli 217 zenye thamani ya zaidi ya milioni 130 kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii wilayani Kakonko mkoani Kigoma.
Mratibu wa huduma za afya ngazi ya jamii wilayani Kakonko Bw. Olela Denishi amesema baiskeli hizo ni kati ya 710 zilizopangwa kutolewa kwa wahudumu hao ambao wanapaswa kuwafikia wananchi na kuwapa huduma za kiafya ikiwemo elimu ya kujikinga na magonjwa mbalimbali
Kwa upande wao baadhi ya wahudumu wa afya ngazi ya jamii wilayani Kakonko wakizungumza na Redio Kwizera baada ya kukabidhiwa baiskeli hizo wameishukuru serikali pamoja na kampuni hiyo huku wakiahidi kufanya kazi kuhakikisha wananchi wanapata huduma ipasavyo
Aidha serikali inaendelea na mpango wa kutoa mafunzo kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii wilayani Kakonko ambapo hadi sasa wahudumu wa afya miambili kumi na nane kati ya mia saba na kumi waliochaguliwa tayari wamepatiwa mafunzo hayo.