Rapa wa Tanzania Webiro Wasira maarufu “Wakazi” amezungumzia taarifa kuhusu uwepo wa hukumu katika kesi ya Clayton Chipando maarufu “Baba Levo” dhidi yake, huku akieleza kuwa hukumu hiyo ilitolewa upande mmoja (Ex Parte).
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Wakazi amesema tayari amemkabidhi Wakili Peter Kibatala kushughulikia mchakato wa kutengua hukumu hiyo kwa hati ya dharura, na kwamba kwa sasa suala hilo lipo mikononi mwa wakili wake.
Aidha, Wakazi amewaomba watu kutoendelea kumtafuta ili atoe maoni kuhusu suala hilo, akieleza kuwa masuala ya kisheria yanayoendelea hayapaswi kujadiliwa kwenye mitandao ya kijamii kwa kuwa yanaweza kuwa na athari za kisheria.
Amesema kuwa taarifa rasmi kwa umma zitatolewa na Wakili Kibatala kwa namna na wakati atakaouona unafaa kulingana na taratibu za taaluma yake.
Mwisho, Wakazi alishukuru na kusema kwa sasa anaendelea na shughuli zake nyingine.
