
Jumla ya wakazi 6,364 wa kata ya Inyara wilayani Geita mkoani Geita wanatarajia kunufaika na mradi wa maji wenye thamani ya shilingi milioni 463.9 ambao umezinduliwa na mbio za mwenge jana Septemba 1
Mradi huo wa skimu ya Inyara ulikuwa unatekelezwa kwa fedha za kupambana na uviko- 19
mradi huo umejengwa na mkandarasi M/S PET kwa usimamizi wa wakala wa maji safi na usafi wa mazingira vijijini wilaya ya Geita RUWASA na kukabidhiwa kwa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Geita GEUWASA kwa ajili ya uendeshaji
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa 2025 Ismail Hussi amepongeza RUWASA kwa kusimamia ujenzi wa mradio huo
Aidha Hussi amewataka wananchi kuutunza mradi huo ili uendelee kuleta tija iliyokusudiwa.