
Zaidi ya wakufunzi 70 wa idara ya Afya Mkoani Kigoma wametunukiwa vyeti vya kuhitimu mafunzo ya ukufunzi katika eneo la Ufafanuzi wa thamani na mabadiliko ya mtazamo VACAT yakiwa na lengo la kuwasaidia wananchi wanaoathirika na vitendo vya ukatili
Akifunga mafunzo hayo yaliyodumu kwa muda wa siku 13 na kugawa vyeti kwa wahitimu Mganga Mkuu Mkoa wa Kigoma Dk. Damas Kayera amewataka wakufunzi hao kwenda kuyafanyia kazi waliyoelekezwa na kuhakikisha wanazalisha walimu wengi zaidi katika sekita ya Afya ili kuweka huduma bora na wezeshi kwa wanajamii.
Akizungumza Kwa Niaba ya Shirika la IRC ambao ni waandaaji wa mafunzo hayo Dk. Ayoub Kasato ameiomba wizara ya Afya kuendelea kutoa ushirikiano katika kuhakikisha wataalamu wengi wanazaliwa kupitia mafunzo hayo