
Wakulima wilayani Biharamulo mkoani Kagera wameshauriwa kutumia mbolea bora ya asili kwa ajili ya kupandia na kukuzia pamoja na kuboresha mashamba ili kupata mazao yenye ubora badala ya kutumia gharama kubwa kuagiza mbolea ya viwandani.
Afisa kilimo wa halmashauri ya wilaya ya Biharamulo Bw. Deus Mashang`ombe amesema hayo wakati akizungumza na Radio kwizera juu umuhimu wa wakulima kutumia mbolea ya asili ili kupunguza gharama zinazowakabili wakulima kwa ajili ya kununua mbolea za viwandani.
Amesema ili kuzalisha mbolea ya asili kila kaya inapaswa kuchimba shimo kwa ajili ya kuhifadhi taka hasa maganda ya ndizi, kinyesi cha kuku, mbuzi na ng`ombe ambayo in akiwango kikubwa cha virutubisho vya udongo wa mbolea tofauti na mbolea ya viwadani.
Baadhi ya wakulima akiwemo Saimon Joseph ,Anord Anatory wamesema maafisa ugani wa wilaya, kata na vijiji wana wajibu wa kutoa elimu kwa wakulima ili kufahamu namna ya kuzalisha mbolea ya asili