Mkoa wa Tabora umeanza rasmi kuuza korosho zake kwa mfumo wa mnada, hatua inayotarajiwa kufungua fursa mpya za kiuchumi kwa wakulima wa zao hilo.
Uzinduzi wa mnada huo umefanywa na Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Upendo Wella na kusisitiza umuhimu wa wakulima kuzingatia ubora wa korosho kuongeza thamani na ushindani wa zao hilo sokoni.
Bi Walle amewataka wakulima kutumia fursa ya masoko yanayopatikana kupitia mfumo wa mnada kujiongezea kipato na kuchangia ukuaji wa uchumi wa Mkoa wa Tabora.
Hatua hiyo inatajwa kuwa ya kihistoria kwa Mkoa wa Tabora, ikiwa ni mara ya kwanza kuuza korosho tangu zao hilo lilipoanza kulimwa mkoani humo.
Baadhi ya wakulima wameeleza matumaini yao kuwa hatua hiyo itachochea uzalishaji zaidi wa korosho na kuongeza mapato yao na ya mkoa.
