
Wakati awamu ya kwanza ya udahili wa shahada ya kwanza likifungwa jana jumla ya waombaji 116,596 wamedahiliwa katika taasisi 88 za elimu ya juu kwa mwaka wa masimu 2025/2026.
Katibu mtendaji wa tume ya vyuo vikuu Tanzania Profesa Charles kihampa amesema kati ya hao 67,576 wamechaguliwa katika chuo kimoja,hivyo wanatakiwa kujithibitisha katika chuo kimoja ndani ya siku 19 kuanzia jana hadi septemba 21,2025.
Hata hivyo kwa wale ambao hawajapata nafasi katika awamu ya kwanza kuwania nafasi hizo udahili wa awamu ya pili umeanza jana hadi tarehe 21 septemba 2025.