
Baadhi ya wakazi wa wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera wameiomba serikali kupitia tume huru ya uchaguzi na vyama vya siasa kutoa elimu na kuhamasisha wananchi kujitokeza kushiriki uchaguzi mkuu wa kuwachagua madiwani, wabunge na Rais.
Miongoni mwa wadau hao Bw. Mbelwa Petro na Josephati Kasusura wamesema hayo wakati wakiongea na Radio Kwizera na kusisitiza kuwa elimu kwa wananchi inahitajika ili kufahamu, faida na madhara ya wananchi kutoshiriki uchaguzi mkuu.
Mkuu wa wilaya ya Biharamulo SACP. Advera Bulimba amesema wananchi waendelee kuwa watulivu muda ukifika wataendelea kupewa elimu na maelekezo na mamlaka husika ili uchaguzi ufanyike wa amani na utulivu.