
Wananchi katika kijiji cha Ilangasika kata ya Lwamgasa wilayani Geita Mkoani Geita wamesema wanalazimika kutumia maji ya mto na wanyama kutokana na kukosekana maji safi na salama katika kijiji hicho.
Wameeleza hayo Wakizungumza na radio kwizera kijijini humo ilipo watembelea kwa lengo la kujua hali ya upatikanaji wa huduma za kijamii ikiwemo maji safi na salama.
Wamesema changamoto hiyo ni ya muda mrefu sasa, wakitumia maji ya mto Nyikonga ambapo asilimia kubwa wanyama hutumia mto huo kwa ajili ya maji na kwamba hali hiyo huwaweka katika hofu ya kukumbwa na magonjwa.
Kwa upande wake diwani wa kata ya lwamgasa Bw. Joseph Masalu akizungumza na radio kwizera juu ya suala hilo kwa njia ya simu amekiri uwepo wa changamoto hiyo na kwamba kwa sasa kuna kisima kimoja tu kinachotumiwa na wananchi huku akiwatoa wasisi wananchi kuifatilia kwa ukaribu changamoto hiyo.