
Wakazi wa majimbo ya uchaguzi ya Chato Kusini na Kaskazini wilaya ya Chato mkoani Geita wameshauriwa kujiepusha na vitendo vya kupokea na kutoa rushwa ili kuwachagua viongozi wanaotaka udiwani na ubunge kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.
Ushauri huo umetolewa na mwenyekiti wa kamati ya amani inayoundwa na viongozi wa dini mbalimbali wilayani humo Shekhe Abdulahman Ismail, wakati akizungumza na Redio Kwizera juu ya athari za rushwa katika uchaguzi wa viongozi.
Amesema licha ya rushwa kuwa ni kosa kisheria bado hata vitabu vitakatifu vya dini zote vimekataza jambo hilo ambapo amewaasa wananchi kuhakikisha siku ya uchaguzi wanawachagua viongozi watakaoshughulika na matatizo ya kijamii.
Baadhi ya wakazi katika majimbo hayo ya uchaguzi, Filmon Msanuzi, Egbert Ntahondi na Ezekiel Magadulla wamepongeza ushauri huo na kuwaomba viongozi wa dini kuendelea kuhubiri