Wananchi wilayani Ngara mkoani Kagera wametakiwa kuendelea kuilinda na kuiendeleza miradi mbalimbali ya mitambo ya kuzimiamoto ili iendelee kuwanufaisha na kuwasaidia pindi majanga ya ajali yanapotokea katika jamii
Hayo yameelezwa na naibu katibu mkuu Wizara ya mambo ya ndani ya nchi Dkt Maduhu Kazi wakati wa hafla ya kukabidhiwa mtambo wa zimamoto na uokoaji uliofadhiliwa na mradi wa umeme Rusumo ( RUSUMO POWER COMPANY LIMITED)kwa jeshi la zimamoto wilaya ya Ngara.

Dkt Kazi amesema kuwa serikali inaendelea kuweka juhudi katika kuhakikisha kuwa jeshi la zimamoto linapata mitambo mikubwa ya zimamoto ili kurahisisha kazi ya zimamoto na uokozi.
Naye mwakilishi wa shirika la Rusumo Power Company Limited amesema kuwa katika kuboresha nafasi ya kutoa huduma bora Kwa jamii wameongeza jitihada za kuondoa msongamano wa changamoto mbalimbali zinazoikumba jamii Kwa njia za utawala,kuongeza shule, vituo vya afya, vyanzo vya maji, na barabara.
Aidha shirika la RPCL limewekeza katika kuongezea magari ya zimamoto ambapo Moja wapo limekabidhiwa rasmi wilayani Ngara mkoani Kagera kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania.
Naye kamishna wa jeshi la zimamoto na uokoaji divisheni ya oparesheni Happyness Shirima ameishukuru serikalikupitia wizara ya mambo ya ndani kwa jitihada ambazo zinafanyika ili kuhakikisha kuwa changamoto ambazo zinajitokeza zinatatuliwa kwa wakati
