
Katibu tawala wilaya ya Ngara Bi. Hatujuani Ally amewataka wananchi kuilinda na kuitunza misitu ya asili ili waweze kuzalisha asali yenye ubora zaidi kuliko misitu ya kupandwa na amesema kuwa kwa sasa asali ya Tanzania inasoko kubwa duniani
Ameyasema hayo wakati wa semina ya uhifadhi wa misitu iliyoandaliwa na wakala wa misitu TFS wilayani humo ambapo amesema uchomaji wa misitu unahatarisha uzalishaji wa asali yenye ubora unaohitajika
Naye Afisa biashara wilaya ya Ngara Bwn Privanus Katinhila amewataka wafanyabiashara ya mazao ya misitu wilayani Ngara kuendelea kufata utaratibu wa Kupata leseni za usafirishaji mazao hayo ili kuepukana na usumbufu unaoweza kujitokeza.
Amesema kumekuwa na changamoto ya wafanyabiashara kutokufata utaratibu uliowekwa wa kuapata leseni na baadae kuanza kulalamikia viongozi kutowatendea haki.
Naye Musa Mlonga ambaye ni Mhifadhi misitu wilaya ya Ngara amesema kuwa lengo la semina hiyo ni kuwahamasisha wadau na wavunaji wa mazao ya misitu waweze kufata utaratibu na miongozo ya serikali.
Afisa wa ufugaji nyuki wilaya ya ngara Agrey Shimwela ambaye ni ameleza faida ambazo zinaweza kupatikana kupitia ufugaji wa nyuki kama vile upatikanaji wa asali ambayo inafaida nyingi kwa wananchi kama kutibu magonjwa mbalimbali.