Mke wa Juma Jux, Priscy, amemjibu shabiki mtandaoni baada ya kumshangaa kwa kurudia viatu vyake vya #JimmyChoo.
Shabiki aliuliza kama viatu hivyo ni vile Priscilla alivaa kwenye harusi yake.
Priscy amesema kwa busara na ujasiri; Kuwa “Kizazi cha wasichana wenzangu kipo kwenye uongo, wakifikira ninaweza kuvaa kiatu cha Jimmy Choo mara moja tu kwa sababu sasa nina mashabiki wengi.
Aidha ameongeza hii ndio sababu hasa wasichana wengi wanajisikia kushinikizwa na mitandao ya kijamii kufuata kiwango kisicho halisi. ‘wanajilaziimisha kuwa wasichana wakubwa wenye nguvu!’ lakini mara nyingi hawana uwezo wa kifedha kuunga mkono aina ya maisha wanayotaka..
Kumbuka: Maisha yangu yataendelea kama ninavyotaka. Mradi tu familia yangu, marafiki, na mashabiki wa kweli wanafurahia, maoni ya wengine ni kelele tu.”
Priscy ameonyesha kuwa maisha yake yanaendeshwa na furaha ya familia, marafiki, na mashabiki wa kweli, na maoni ya wengine hayana uzito kwake.