
Na, Samuel Mausunzu
GEITA
Wazazi na walezi mkoani Geita wametakiwa kuwakatia kadi za bima ya afya watoto wao ili kuwahakikishia uhakika wa matibabu wakati wote
Meneja wa mfuko wa taifa wa bima ya afya mkoa wa Geita Bw. Elius Odhiambo ameeleza hayo wakati akiongea na redio kwizera juu ya mkakati wa matibabu kwa watoto hasa waliopo shuleni na vyuoni
Amesema serikali inaendelea na mpango wa bima kwa watoto ambao huwasaidia pale wanapokutana na changamoto za kiafya wakiwa masomoni
Mkuu wa mkoa wa Geita Martine Shigela akiwa kwenye kituo cha kulelea watoto yatima cha moyo wa huruma amesema wakati serikali ikiendelea kuboresha huduma za afya, jamii nayo ione wajibu wa kuyahudumia makundi mbalimbali ambayo hayana uwezo wa kugharamia bima za afya hasa baadhi ya wanafunzi ambao familia zao ni duni kiuchumi