
Wakazi wa kijiji cha Nyakagomba wakiwemo wazee wilayani Geita mkoani Geita wameomba ofisi ya vitambulisho vya taifa NIDA kuwafikia na kuwapatia huduma hiyo ili waweze kutimiza shughuli zinazohitaji vitambulisho hivyo
Mmoja wa wazee wakijiji hicho Bw. Revocatus Ernest ameeleza hayo katika mkutano wa mkuu wa mkoa wa kusikiliza kero za wananchi ,na kudai kuwa watoto wao wanashindwa kutimiza vigezo katika kutafta ajira kutokana na kutokuwa na vitambulisho vya taifa
Kwa upande wake meneja wa vitambulisho vya taifa NIDA mkoa wa Geita bw. Ramadhan Charles amesema tayari wameshandaa utaratibu wa kuwafikia wananchi wa kijiji hicho pamoja na vijiji vingine ili wapate viutambulisho hivyo