Waziri wa Afya wa zamani wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Jenista Joakim Mhagama, amefariki dunia leo tarehe 11 Desemba 2025 jijini Dodoma.
Taarifa ya kifo chake imetolewa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Azzan Zungu, kupitia Kitengo cha Mawasiliano cha Ofisi ya Bunge.
Aidha amewapa pole Wabunge wa bunge la Tanzania, familia ya marehemu, ndugu, jamaa na wananchi wa Jimbo la Peramiho kutokana na msiba huo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia ya marehemu inaendelea kuratibu mipango ya mazishi, na taarifa zaidi zitatolewa kadri taratibu zitakavyokamilika.
Marehemu Mhagama aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini, zikiwemo nafasi kadhaa za uwaziri. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) mwaka 2015 katika Serikali ya Rais John Magufuli, kabla ya kuhamishiwa Ofisi ya Rais kushughulikia tawala Bora mwaka 2022 na katika awamu ya sita alikuwa waziri wa Afya kabla ya wizara hiyo kushikiliwa na wazie Mohamed Mchengerwa 2025.
Aidha Taarifa ya Spika wa Bunge la Tanzania haijaeleza chanzo cha Kifo hicho.