Rapa maarufu wa Marekani WizKhalifa amehukumiwa kifungo cha miezi 9 gerezani nchini Romania baada ya kupatikana na hatia ya kumiliki na kutumia dawa za kulevya (bangi), tukio lililoibuka zaidi ya mwaka mmoja baada ya kushuhudiwa akitumia dawa hiyo jukwaani wakati wa tamasha la Beach, Please! Festival huko Costinesti, Romania, mwaka Julai 2024.
Kulingana na sheria za Romania, kumiliki hata kiasi kidogo cha bangi kwa matumizi ya kibinafsi ni kosa la jinai, na hukumu inaweza kuwa kati ya miezi 3 hadi miaka 2 au faini, kulingana na uzito wa kesi.
Hadi sasa haijafahamika wazi iwapo Wiz Khalifa atalazimika kutumikia kifungo hicho lini huku ikisubiriwa kesi ya rufaa au suala la uhamisho wa kifungo, kwa kuwa yeye ni raia wa Marekani na hana makazi ya kudumu Romania.
Tukio hili limezua mjadala kuhusu tofauti za sheria za dawa za kulevya katika nchi mbalimbali, hasa kwa wasanii wanaosafiri ulimwenguni na kushiriki tamasha bila kufahamu vigezo vya kisheria vya nchi wanazozitembelea.