
Mchakato wa kumchagua Papa katika Kanisa siyo mchakato au shughuli ya kisiasa bali shughuli ya kiroho, inayofanywa kwa muktadha wa sala na tafakari kutoka mwanzo hadi mwisho. Shughuli hii inaongozwa na Roho Mtakatifu zaidi tofauti kabisa na namna ya kidunia kama tudhanivyo. Kwa hiyo ni vigumu kutabiri kuwa Papa ajaye atakuwa yupi ama atatoka bara lipi kwa sababu Kanisa ni Moja, Takatifu, Katoliki na la Mitume.
Kwa mujibu wa mwongozo wa Kanisa, umoja wa Makadinali utaanza Kongamano lake la kumpata mrithi wa Papa Francisco wiki hii Jumatano tarehe 7 Mei 2025. Ungana nasi kuzijua hatua hizo!
Zifuatazo ni hatua za kumpata mrithi wa papa!
- KWANZA, ASUBUHI YA TAREHE 7 MEI, Makadinali wote (wapiga kura na wasio wapiga kura) wataadhimisha Misa iitwayo Pro Eligendo Pontifice, Misa ya Roho Mtakatifu. Misa hii huadhimishwa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro na itaadhimishwa na kiongozi Mkuu wa Makadinali, Kadinali Giovanni Battista Re, akisaidiwa na Makamu Mkuu wake (Kadinali Leonardo Sandri) na kadinali Shemasi-mkuu (Protodeacon) akiwakilisha nafasi ya uongozi na huduma.
- KISHA MCHANA, saa kumi na moja jioni, wateule wote wa Kadinali, pamoja na wasaidizi wachache walioidhinishwa (k.m. Katibu wa umoja wa Makadinali, Mwaadhimishi Mkuu wa Maadhimisho ya Liturujia ya Kipapa, Waadhimishi wawili wa adhimisho na Msakristia) watakula na kutia saini kiapo cha usiri na uaminifu wakati wa uchaguzi.
- Makadinali watafanya MAANDAMANO KUINGIA kwenye Kapela ya Sistine. Wataingia wakiimba Litania ya Watakatifu na Veni Creator Spiritus (Njoo Roho Mtakatifu) wakiongozwa na Mwadhimishi Mkuu wa Maadhimisho ya Liturujia.
- Makadinali-wachaguzi hula KIAPO cha usiri ambacho kinasimamiwa na Mwadhimishi Mkuu wa Maadhimisho ya Liturujia; kila Kadinali-mchaguzi anaweka mkono wake juu ya Kitabu cha Injili na kuapa kwa usiri kabisa.
- Baadaye, Mwadhimishi Mkuu wa Maadhimisho ya Liturujia anatangaza; Omnes za ziada! na wote wasio wachaguzi (isipokuwa mhubiri wa tafakari ya pili) wanatoka nje ya Kapela.
- Mhubiri mkuu wa Kongamano ambaye pia ni Mhubiri wa Kaya ya Papa (Padre Raniero Cantalamessa, O.F.M.Cap.), Atawapa wapiga kura Tafakari juu ya uzito wa kazi iliyo mbele yao.
- Kisha Upigaji Kura utaanza: Siku ya kwanza, tarehe 7 Mei, kura itafanyika alasiri moja tu.
- Kwa kawaida Makadinali hupiga kura mbili/yaani wanapiga kura mara mbili kila asubuhi na mara mbili kila mchana (hadi mara nne kwa siku).
- Makadinali watatu wanachaguliwa kujumlisha kura (“wachunguzi”), watatu kukagua hesabu (“wahakiki”), na watatu “infirmarii” kukusanya kura kutoka kwa wapiga kura ambao hawawezi kujitokeza; wote wameteuliwa na kiongozi mkuu anayejulikana kama “Dean” (Kiongozi wa makadinali).
- Mara tu upigaji kura unapoanza, kila mteule wa kadinali anatumia kanuni hii “Namwita shahidi wangu Kristo Bwana … kwamba kura yangu ni kwa ajili ya yule ambaye ninaridhia kwamba anafaa kuchaguliwa kuwa papa.”
- Ili Kardinali awe Papa ni lazima apate theluthi mbili ya kura. Kwa kuwa mwaka huu kuna makadinali wachaguzi- wapiga kura ni 135, theluthi mbili ni kura 90. Ikiwa hakuna atakayefanikisha idadi hiyo ya kura, wanafanya duru ya pili. Ikiwa bado hakuna anayepata theluthi mbili, wanapeleka kura hizo kwenye bomba la moshi na huchomwa ili kutoa “moshi mweusi.” (Kwa Kiitaliano inaitwa “fumata nera”)
- Iwapo Kadinali- wapiga kura watapiga kura mara moja na kupata theluthi mbili basi kura zitachomwa na kisha kuonekana moshi Mweupe (“fumata bianca”); na tunaye Papa.
- TANBIHI: Ikiwa baada ya siku tatu kamili za kupiga kura hatumpati Papa, mapumziko ya siku moja yanaruhusiwa kwa sala na kutafakari (kwa kawaida huongozwa na Mhubiri yule yule wa Kongamano ama Conclave), na mijadala mingine isiyo rasmi kati ya wapiga kura (bado wakiwa chini ya kiapo). Mkandidati akishafikisha theluthi mbili: Kiongozi Mkuu, atamhoji akimuuliza: “Je, unakubali kuchaguliwa kwako kama Papa Mkuu?” Anaposema “Accepto,” au ‘Ninakubali’ mkuu atamuuliza tena: “Unataka kuitwa kwa jina gani?”
- Mgombea mpya huchagua na kutoa jina la mtakatifu au Papa wa zamani ambalo angependa kuchukua baada yake. Kumbuka Mapapa hawatajwi kwa majina yao bali jina hili jipya kama Papa Francis alikuwa Kadinali Jorge Mario Bergolio. (Hakuna Papa aliyewahi kuchukua jina la Petro, Papa wa kwanza kwa heshima. Baada ya yote, ofisi ya Papa ni ile ya Petro).
- Kisha Mwadhimishi wa Maadhimisho ya Liturujia ya Kipapa anafanya kazi kama mthibitishaji, kuandika na kutia saini hati rasmi ya kukubalika, pamoja na Maafisa wawili ambao ni mashahidi mashahidi.
- Papa mpya anapelekwa kwenye Kapela nyingine “KAPELA YA MACHOZI” ili kupokea mshtuko. Kisha anavishwa Kanzu nyeupe ya Kipapa na kofia nyeupe na pete mpya ya mvuvi. Kumbuka, pete ya mvuvi ya Papa aliyetangulia inaharibiwa mara tu baada ya kifo chake (au baada ya kujiuzulu).
- Papa mpya anarudi kwa Makadinali ambapo wanamwombea na kutoa sala ya shukrani. Pia wanaahidi utii kwake. Wakati huo, Moshi Mweupe tayari umepanda na kengele zinalia na umati wa watu uwanjani na ulimwengu unamngojea kuonekana kwenye balcony (Baraza) ya dirisha la Basilica ya Mt. Petro
- Katika Rituale ya Kiroma, Kadinali Shemasi mkuu ni Kadinali Protodeacon wa Kanisa Takatifu la Roma. Ana bahati ya kutangaza uchaguzi na jina la papa mpya (mara tu atakapotawazwa kuwa uaskofu). protodeacon (shemasi mkuu), Kadinali Maberti, atatokea kwenye balcony ya kati ya Basilica ya Mtakatifu Petro na kusema: “Annuntio vobis gaudium magnum: Habemus Papam!” yaani; “Nakutangazia kwa furaha kubwa kwamba tuna Papa!” Kisha mapazia yanafunguka na Papa mpya anatambulishwa kwa jina lake na kupewa jina lake rasmi, kwamba ataitwa Papa hivi na hivi! Baada ya makofi kutoka kwa watu, Papa mpya anatoa baraka za “Urbi et Orbi” kutoka kwenye dirisha la Basilica ya Mt. Petro.
- Ndani ya siku (mara nyingi ndani ya wiki moja), Papa mpya anaadhimisha Misa ya Uzinduzi wa huduma yake ya Petrine katika Basilica ya Mtakatifu Petro au Uwanja, inayohudhuriwa na wakuu wa nchi na Chuo cha Makadinali. TANBIHI: Ukuu wa Petro, pia unajulikana kama ukuu wa Petrine (kutoka kwenye tafsiri ya Kilatini: Petrus, “Peter”), ni nafasi ya ukuu ambayo inahusishwa na Petro kati ya Mitume Kumi na Wawili.
- TANBIHI: Papa hajawekwa rasmi kuwa Papa. Anakuwa Papa MARA baada ya kuchaguliwa na ANAPOKUBALI. Kumbuka Sakramenti ya Kuwekwa wakfu ina ngazi tatu – Ushemasi, Ukuhani na Uaskofu. Ikiwa tayari mgombea aliyechaguliwa tayari ni Askofu hakuna Daraja. Lakini katika tukio lisilowezekana kwamba mgombea ni Padre, ni lazima awekewe askofu kwanza. Hata hivyo, katika hali ya kawaida – hasa siku hizi, mapapa wanachaguliwa kati ya makadinali ambao tayari wana utimilifu wa ukuhani (tayari maaskofu). Kwa hiyo wakati wa Misa ya uzinduzi, Papa anapokea PALLIUM: hii ni ngozi ya kondoo wanayovaa mabegani mwao ili kuonyesha jukumu la uchungaji. Pallium inatolewa kwa Maaskofu wakuu katika adhimisho la Sikukuu ya Watakatifu Petro na Paulo. Kwa hiyo akiwa Papa, anapokea Pallium ya Upapa wakati wa Misa ya uzinduzi.
- Baadaye (kwa kawaida ndani ya miezi), anachukua rasmi kanisa lake kuu kama Askofu Mkuu wa Roma; Basilika Kuu la Mt. Yohane Lateran.
- Haya ni baadhi ya mambo ambayo Makardinali watafanya Tarhe 7 Mei 2025 wakati wamchakatomzima wa kumpata Papa Mpya ajaye katika Kanisa.
Imetafsiriwa na Fr. Didmus Didasi, SJ.