
Cardinals attend the Holy Mass, celebrated for the election of the new pope, presided over by the Dean of the College of Cardinals, Cardinal Giovanni Battista Re, in St. Peter’s Basilica, at the Vatican, May 7, 2025. REUTERS/Murad Sezer
Hivi sasa, kuna Makadinali 252 kati yao 135 wako chini ya umri wa miaka 80. Kwa hiyo hawa ndio Makadinali watakao fanya uchaguzi wa kumpata Papa mpya na ambao hawatofanya uchaguzi huo ni wenye umri wa miaka 80 au Zaidi ambao ni jumla ya 117.
Zijue nafasi za makadinali 252 na Majiundo yaliyofanywa na Mababa Watakatifu:
- Nafasi 41 ziliundwa na Papa Mtakatifu Yohane Paulo II. Miongoni mwa hao (5) ni Kardinali Wapiga kura huku 36 wakiwa wasio wapiga kura.
- Nafasi 62 ziliundwa na Papa Benedict XVI. Miongoni mwao (22) ni Kardinali Wapiga kura huku (40) ni Kardinali-wasio wapiga kura.
- Nafasi 149 ziliundwa na Papa Francis. Miongoni mwao (108) ni Kardinali wapiga kura huku 41 ni Kadinali wasio wapiga kura.
NAMBA ZA MAKADINALI KWA MABARA YA ASILI
- Ulaya: 114 jumla | Wapiga kura (53) | wasio wapiga kura 61
- Asia: 37 jumla | Wapiga kura 23 | wasio wapiga kura 14
- Amerika ya Kusini: 32 jumla | Wapiga kura 17 | wasiowapiga kura 15
- Afrika: 29 jumla | Wapiga kura (18-1) | wasio wapiga kura 11
- Amerika Kaskazini: 28 jumla | Wapiga kura 16 | wasio wapiga kura 12
- Amerika ya Kati: 8 jumla | Wapiga kura 4 | wasio wapiga kura 4
- Oceania: 4 jumla | Wapiga kura 4 | 0 wasio wapiga kura
Nchi Zinazoongoza kwa Idadi ya Wapigakura: Italia: 17 | Marekani: 10 | Brazil: 7
Kardinali Mzee zaidi ni Angelo Acerbi kutoka Italia na atatimiza miaka 100 mnamo Septemba 23.
Kadinali mdogo zaidi ana umri wa miaka 45. Yeye ni Kardinali Mykola Bychok kutoka Australia (amezaliwa Februari 1980)
Mgawanyiko wa kijiografia wa wapiga kura unaonyesha kuwa hakuna kambi mbili za bara peke yao zinaweza kumchagua papa. Hii inahakikisha kwamba papa mteule lazima awe na rufaa ya kimataifa.
KUMBUKA: Makadinali wawili hawatoweza kupiga kura kwa sababu za kiafya. Kardinal Antonio Cañizares Llovera Kutoka Jimbo Kuu la Uhispania. Wa pili ni Kadinali Cardinal John Njue, aliyekuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki Nairobi nchini Kenya. Sababu hii inafanya Makadinali wapiga kupungua kwa idadi na kufikia 133.
Ili Kardinali awe Papa ni lazima apate theluthi mbili ya kura. Kwa kuwa mwaka huu kuna makdinali wateule- wapiga kura ni 133, theluthi mbili ni kura 89. Ikiwa hakuna atakayefanikisha idadi hiyo ya kura, wanafanya duru ya pili. Ikiwa bado hakuna anayepata theluthi mbili, wanapeleka kura hizo kwenye bomba la moshi na huchomwa ili kutoa “moshi mweusi.”
Iwapo Kardinali wapiga kura watapiga kura mara moja na kupata theluthi mbili basi kura zitachomwa na kisha kuonekana moshi Mweupe kuonesha tunaye Papa.