Jeshi la zimamoto na uokoaji Wilayani Muleba Mkoani Kagera limewataka watega senene kuchukua taadhari ya majanga ya moto wakati wa shughuli zao.
Kaimu Mkuu wa Jeshi la zimamoto Wilaya ya Muleba, Slyvester Mfumu amesema kipindi hiki kumekuwa na changamoto ya kukatika kwa umeme mara kwa mara kwasababu ya watega senene kutofuata utaribu wa kuunganishiwa umeme.
Amesema kuwa wanatoa elimu kwa wakzi wa kata ya muleba kuchukua tahadhari kwasababu ya kujiunganishia umeme kiholela kwa ajili ya kutega senene nakuhatarisha usalama wa maisha yao.
Baadhi ya wategaji wa Senene wamesema kutokuwa na elimu yoyote ya umuhimu wa kutega senene kwa kufuata utaratibu kunasababisha baadhi ya nyumba kuungua na moto.
Biashara ya Senene Mkoani Kagera hasa katika miji ya Manispaa ya Bukoba,Bunazi,Kayanga Muleba na maeneo mengine imejizolea umaarufu zaidi hata kwa mikoa mingine kutokana na usabazaji wa bidhaa hiyo kwa walaji.

Njia za uaandaji wa Senene Mkoani Kagera zinaibuka kila kukicha na kuwa katika ushindani wa hali ya juu zaidi ya Biashara hiyo.
Lakini kutokana na Biashara ya Senene kukua kila mmoja anahitaji kufanya kazi hiyo na kujikuta wengine wanavunja utaratibu wa kuunganishiwa umeme na kuhatarisha usalama wao na jamii kwa ujumla kutokana na mfumo wa umeme kupata hitrafu.
Senene mkoani kagera kwa mjibu wa Tamaduni ni chakula kinacho thaminiwa zaidi na makundi yote hata walioko mikoani wakiwa na asili ya mkoa wa Kagera.