Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amesema shughuli za Mama Lishe na Baba Lishe zinapaswa kutambuliwa na kuheshimiwa kutokana na mchango mkubwa wanaoutoa katika maisha ya kila siku ya Watanzania.
Rais Samia amebainisha katika Kongamano la Kitaifa la Mamalishe na Babalishe, lililofanyika leo Jumanne Aprili 21, 2026 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
Amesema upo umuhimu wa kuwapa Mama Lishe mafunzo ya ujasiriamali na usimamizi wa mitaji kwasababu wengine wakipata fedha badala ya kufanyia mambo ya msingi ikiwemo kupanua biashara wao wanakwenda kutunzana kwenye vikundi.
Aidha amesema kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira rafiki yatakayowawezesha wafanyabiashara hao wadogo kufanya kazi zao kwa utulivu na usalama, huku akiwataka viongozi wa maeneo mbalimbali kuacha vitendo vya unyanyasaji dhidi yao.
