Wafanyabiashara wa samaki katika soko kuu la Chato wilayani Chato mkoani Geita wameiomba serikali kuwawekea miundombinu bora ya majitaka katika soko hilo ili kuimarisha usafi wa mazingira.
Baadhi ya wafanyabiashara hao Innocent Lata, Sayuni Binamu na Asteria David wametoa ombi hilo wakati wakiongea na Redio Kwizera juu ya changamoto ya kukosena kwa miundombinu hiyo.
Wamesema soko hilo huzalisha taka zinazotokana na samaki ambazo huoza na kutoa harufu mbaya na kwamba wao hushindwa kufanya usafi kwa bidhaa zao kutokana na ukosefu wa miundombinu hiyo.
Insert………..wafanyabiashara samaki.
Kwa upande wake afisa biashara viwanda na uwekezaji katika halmashauri ya wilaya ya Chato Bi. Ester Benjamin amesema kuwa tayari vikao vya kuchakata bajeti ya kukarabati miundombinu hiyo vimefanyika na kwamba hadi disemba 30 mwaka huu ukarabati utakuwa umefanyika.
