
Wadau wa nishati safi ya kupikia nchini wameiomba serikali kuendelea kuharakisha upatikanaji wa teknolojia za kisasa za nishati hiyo hususani maeneo ya vijijini ambako mpaka sasa inadaiwa kuna bado kuna asilimia kubwa ya matumizi ya nishati chafu ya kuni na mkaa
Hayo yamebainishwa jijini Dodoma katika tamati ya mradi wa miaka minne wa programu ya nishati safi ya kupikia nchini (TCCP)ulioanza mwaka 2022 wenye lengo la kuwajengea uwezo makampuni yanayofanya biashara katika sekta ya nishati safi,kutoa ruzuku kwa makampuni ili yaweze kufikisha teknolojia za nishati safi katika maeneo ya vijijini na yaliosahausika.
Wadau hao wamedai kutumia zaidi ya Shilingi Bilioni kumi kuunga mkono juhudi hizo kwa kuwafikia wananchi laki moja na themanini, kutoa ruzuku kwa kampuni kumi na tatu na kusambaza majiko takribani mia tisa ili adhma ya kulinda afya za watu pamoja na kutunza mazingira ifikiwe kikamilifu. niandikie kichwa cha habari
