Kundi la waasi la M23 limetangaza leo kuwa limekubali ombi la Marekani la kujiondoa kutoka mji wa Uvira, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Kujiondoa kwa M23 Uvira kumethibitishwa usiku wa kuamkia December 16, 2025 kupitia taarifa iliyosainiwa na mratibu wa muungano unaojumuisha kundi hilo leo Corneil Nangaa.
Aidha M23 imetoa wito wa kuwekwa kwa mikakati ya kutosha kusimamia mji huo ikiwa ni pamoja na kuondoa wanajeshi, kuwalinda wakazi wa eneo hilo na miundombinu pamoja na kufuatilia makubaliano ya amani kwa kutoegemea upande wowote.
Kundi hilo pia linataka kutekelezwa kwa mapendekezo ya mpango wa amani yaliofikiwa katika mchakato sambamba wa amani wa mjini Doha nchini Qatar yaliyokubaliwa mwezi Novemba lakini ambayo hayajatekelezwa.
Pia limesema kujiondoa kwake Uvira ni ishara ya kujenga imani ili kutoa nafasi ya kufanikiwa kwa mchakato wa Doha