Press "Enter" to skip to content

Kibondo Watakiwa Kudumisha Amani Baada ya Mfungo

πŸ—“οΈ Ijumaa, Machi 14, 2025 | ⏰ 11:00 PM

πŸ“ Kibondo, Kigoma

πŸ“° Wananchi Kibondo Watakiwa Kudumisha Amani Baada ya Mfungo

Serikali wilayani Kibondo mkoani Kigoma imewataka wananchi kudumisha amani iliyopo kwa kujiepusha na vitendo vya uhalifu hata baada ya kumalizika kwa mfungo mtukufu wa Ramadhan na Kwaresma.

Akizungumza katika kikao cha wadau wa maendeleo, Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Kanali Agrey Magwaza amesema baadhi ya wananchi walio katika kipindi cha kufunga, wanapomaliza mfungo wamekuwa wakijihusisha na tabia ambazo si nzuri kwa jamii.

Kanali Magwaza ameongeza kuwa jamii inapaswa kuyaishi mafundisho yanayotolewa na viongozi wa dini ili kupunguza matukio ya uvunjifu wa amani.

Kwa upande wao, baadhi ya wananchi wilayani humo wamesema wataendelea kushirikiana na serikali katika nyanja mbalimbali kwa kuilinda na kuienzi amani iliyopo, ikiwa ni pamoja na kuendelea kuwa wazalendo kwa taifa lao.


Chanzo: RK, Shoraa (Amani)
Mhariri: JR
Tarehe: Machi 14, 2025.

Be First to Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *