Waziri wa Kawi wa Kenya, Opiyo Wanyayi, ameitisha mkutano wa dharura na wauzaji mafuta, saa chache baada ya kufanya mazungumzo na makampuni yanayosambaza mafuta nchini chini ya makubaliano ya ya serikali kwa serikali maarufu G-2-G.
Wandayi amesema atafanya mkutano huo leo huku akiondoa wasiwasi wa uhaba wa mafuta.
Waziri huyo pia amedokeza kuwa serikali inajadiliana na mataifa yanayozalisha mafuta ambayo Kenya ilifikia mkataba wa G-2-G , kama vile ARAMCO ya Saudi Arabia, ili kuhakikisha upatikanaji wa mafuta ya kutosha kwa muda mrefu iwezekanavyo kwa kuzingatia mipango ya dharura.
Haya yanajiri kufuatia mgogoro uliozuka Mashariki ya Kati baada ya Marekani na Israel kuishambulia Iran na kumuua Kiongozi Mkuu wake Ayatollah Ali Khamenei wiki iliyopita.
Iran imekuwa ikilipiza kisasi hatua hiyo kwa kuyashambulia mataifa jirani ya Ghuba ambayo ni mshirika wa Marekani na kufunga Mlango-Bahari wa Hormuz, njia inayotumika kwa usambazaji wa asilimia 21 ya mafuta duniani
