Hadithi ya Akon kuhusu ringtones (milioni ya simu) ni moja ya simulizi zinazofungua macho ya wasanii wengi juu ya biashara ya muziki nje ya kuuza nyimbo kamili.
Akon amesimulia jinsi alivyokuja kugundua kuwa ringtone ya sekunde chache ilikuwa inaingiza mapato makubwa kuliko wimbo mzima, huku mikataba ya mwanzo ikiwa haijaainisha kipengele cha ringtones. Alipolitambua hilo, akaanza kupigania haki zake na kubana wawekezaji kuhusu mikataba ya matumizi ya kazi zake kwenye simu. Hatua hii ilimuweka Akon kwenye kitabu cha Guinness World Record, akiwa msanii ambaye nyimbo zake zimeuzika zaidi kama ringtones.
Kinachovutia zaidi ni kwamba hali kama hiyo iliwahi kutokea pia Tanzania. Kulikuwa na tukio ambapo wasanii wawili walilipwa fidia na kampuni ya mtandao wa simu, baada ya kubainika kuwa nyimbo zao zilikuwa zinauzwa kama ringtones kwa muda mrefu bila wao kuhusishwa rasmi kwenye makubaliano wala kunufaika ipasavyo na mapato hayo.
Haya yote yanaacha somo muhimu kwa wasanii: elewa biashara ya muziki wako na linda haki zako.Wakati huo huo, kuna fursa kubwa ya kuunda nyimbo rafiki kwa mazingira ya watu, zenye hook kali, ujumbe unaogusa maisha ya kila siku, na zinazoweza kutumika kwenye majukwaa mbalimbali ya kidigitali. Muziki sio sanaa peke ya, ni mali; na anayeelewa thamani yake mapema, ndiye anayeshinda