ZAWADI Bashemela

Zawadi Bashemela ni mwandishi wa habari na mtangazaji kwa zaidi ya miaka 20. Kwa kipindi chote hicho ameshiriki kuandaa maudhui ya radio kupitia vipindi na habari ili kuleta mabadiliko katika jamii hasa kwenye nyanja za afya, elimu, siasa, uchumi na utamaduni. Anaamini katika kazi yake jambo kubwa ni kuendelea kuwa nguzo muhimu katika kujenga jamii yenye uelewa, maadili mema, uwajibikaji na kuwa na maendeleo ili kufikia ndoto ya watanzania wengi. "Habari Sahihi Jamii Imara"