Mwanamke wa Uingereza Lucy Harrison aliyeuwawa kwa kupigwa risasi na baba yake alipokuwa amemtembelea nyumbani kwake huko Texas nchini Marekani, uchunguzi umeeleza kulikuwa na mabishano ya kisiasa.
Mwanamke huyo alipigwa risasi Jan 10, mwaka jana baada ya kuwepo mabishano na baba kuhusu Rais wa Marekani Donald Trump, ambaye alikuwa akijiandaa kuapishwa kwa muhula wake wa pili.

Polisi katika mji huo walichunguza kifo cha kijana huyo mwenye umri wa miaka 23 kama mauaji ya bila kukusudia lakini hakuna kesi ya jinai iliyoletwa dhidi ya mwanaume aliyemuua bintiye Kris Harrison baada ya mahakama kuu katika kaunti ya Collin kukataa kumfungulia mashtaka.

Uchunguzi wa kifo cha Lucy Harrison ulianzishwa mapema katika Mahakama ya Cheshire Coroner, ambapo mpenzi wake Sam Littler alielezea kuwepo kwa mabishano makubwa kuhusu Trump

