
Zaidi ya shilingi bilioni 2 zimetumika kujenga miundombinu mipya ya elimu katika wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma, na kutatua changamoto ya watoto kutembea umbali wa zaidi ya kilomita 15 kufuata huduma ya elimu.
Mwenyekiti wa maendeleo ya jimbo la Kakonko ambaye ni mbunge wa jimbo hilo Aloyce Kamamba, akiongea na baadhi ya wakazi wa kata za Nyamtukuza na Muhange, amesema fedha hizo zimetolewa na serikali kwa mwaka 2020-2025.
Amesema kutokana na shule zilizokuwepo awali kutokidhi mahitaji ya watoto wa wilaya hiyo, kwa sababu za umbali na za kijografia, baadhi yao walikatisha masomo jambo ambalo kwa sasa litabaki historia.
Baadhi ya wakazi wa kata ya Muhange na Nyamtukuza akiwemo Tabia Yujen Mikael Ntahondi Pius Kamhanda na pendo Ruvyoogo wamepongeza jitihada za serikali katika utatuzi wa changamoto hiyo na kwamba kwa sasa hakuna mwanafunzi anaetembea umbali wa kilomita 10 kufuata masomo.