Jessie Buckley ameshinda tuzo ya Oscar kipengele cha mwigizaji bora wa kike kwa mara ya kwanza siku ya Jumapili kwa uhusika wake kwenye filamu ya “Hamnet” ambayo ilisababisha karibu kila mtu aliyeiona kutokwa na machozi.
Filamu hii inaliza na muhusika ambaye ni Jessie Buckley ameitendea haki. Ameigiza kama mke wa William Shakespeare, Agnes, katika tamthilia iliyoongozwa na Chloé Zhao.
Hamnet iliyotengenezwa kuakisi maisha ya mwaka 1596 ya familia ya William Shakespeare. Filamu hii inaazungumzia kifo cha cha mtoto wa miaka 11 wa William Shakespeare, Hamnet, na jinsi pigo hili kubwa kwa familia lilivyochochea kutengenezwa kwa filamu ya Hamlet iliyoandikwa na Shakespeare mwenyewe.
Hamnet ni filamu inayoangazia huzuni, ndoa, na maisha ya familia katika familia za Uingereza karne ya 16.
