Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Leo, anatarajiwa kuanza ziara rasmi katika mataifa manne ya Afrika kuanzia Aprili 13 hadi 23, 2026, ikiwa ni safari yake ya tatu ya kitume nje ya Italia tangu aanze uongozi wake.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Holy See Press Office, Papa Leo atatembelea mataifa ya Algeria, Cameroon, Angola na Equatorial Guinea katika safari ya siku 11 itakayohusisha hotuba 10, mahubiri nane na salamu sita katika miji 11.
Ziara hiyo inafuatia safari yake ya mwaka 2025 katika Mashariki ya Kati alipokwenda Uturuki na Lebanon, huku safari nyingine ya Ulaya ikitarajiwa kufanyika Machi 28 mwaka huu katika Monaco.
Ratiba inaonyesha Papa Leo ataanza ziara yake katika Algeria, ambapo anatarajiwa kuwasili katika mji mkuu wa Algiers Aprili 13.
Amina Deogratius Semagogwa (SEMA G)
ni mwandishi wa habari na mtangazaji mahiri wa Radio mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 10 katika tasnia ya habari, Amebobea katika kuandaa na kuendesha vipindi vyenye uzito vinavyolenga kuibua mijadala ya kijamii, hususan katika malezi bora ya watoto na masuala ya utawala bora.
Kupitia kalamu na sauti yake Amina ametunukiwa tuzo zaidi ya 10 za uandishi bora wa habari nchini Tanzania , Amina amejijengea nafasi ya kuwa daraja kati ya jamii na maarifa, akiamini kuwa uandishi wa habari si kuripoti tu bali ni chombo cha kuelimisha, kuhamasisha na kuleta mabadiliko chanya, Ana mtindo wa kipekee unaochanganya weledi, uchambuzi na uwasilishaji unaogusa maisha halisi ya watu.
Kauli mbiu: Sauti ya jamii, dira ya mabadiliko.