
Kocha Mkuu wa klabu ya Bayer Leverkusen, Xabi Alonso, ameiaga rasmi timu hiyo ya Ligi Kuu Ujerumani-Bundesliga baada ya kuitumikia kwa zaidi ya miaka miwili.
Kwa muda sasa Alonso amehusishwa kuondoka Leverkusen ambapo sasa tetesi zinasema Alonso amesaini mkataba wa miaka mitatu Real Madrid ya Hispania hadi 2028.
Taarifa ya Leverkusen imeeleza “Baada ya miaka mwili na nusu na kipindi cha mafanikio zaidi katika historia ya klabu, kocha wetu mkuu, Xabi Alonso ataondoka #Bayer04 mwisho wa msimu”
Alonso ameshinda mataji mtatu akiwa kocha Leverkusen ambayo ni Bundesliga na Kombe la DFB msimu wa 2023/24 na Supercup 2024.