
Na, Jerome Robert
GOMA
Kundi la waasi la M23 lichukizwa na hatua za vikosi vya SADC vya Kivu Kaskazini, kwa kukiuka mkataba wa makubaliaono kwa kushirikiana na jeshi la FARDC kutekeleza mashambulizi katika maeneo kadhaa ya mji wa Goma.
Kupitia taarifa walioichapisha mapema leo M23 wanaoshirikiana na washikadau wengine kwenye muungano wa Congo River Alliance, wameeleza hayo kutokana na kile wamekitaja kuwa hatua zinazohatarisha maisha ya raia katika mji huo wa Goma.
Msemaji wa kundi hilo Lawrence Kanyuka wamechukizwa na mashambulizi ya Aprili 11 na kusema kuwa yanatishia moja kwa moja, hali ya usalama wa raia katika eneo hilo.
Aidha, M23 sasa inasema italazimika kuchukuwa hatua na kujibu mashambulizi dhidi yao ikiwa itaendelea kuchokozwa.