SONY DSC
Baraza kuu la maaskofu wa kanisa katoliki nchini DRC limeonya kuhusu mabadiliko ya katiba nchini humo na kuwataka viongozi kuwa makini kwa maamuzi watakayo yachukua.
Akizungumza jana na vyombo vya habari mjini Kinshasa katibu wa baraza la maaskofu Mwashamu Askofu Donatien Nshole amesema kuwa wakati huu ambapo nchi imegawanyika na vita, si muda muafaka wa kuwepo mabadiliko ya katiba.
Amesema kubadili katiba huku mashariki mwa DRC ikiwa imedhibitiwa na waasi ni jambo ambalo linaitaji umakini mkubwa, kwani linaweza kuvunja umoja wa kitaifa na kuwapa nguvu waasi wa M23 ili waendelee kushambulia miji mingeni ya DRC.
Kauli hiyo ya viongozi wa kanisa katoliki imekuja kutokana na mvutano kati ya wanasiasa ambapo tawala cha UDPS kimeanza kampeni ya kushawishi wananchi kuhusu mabadiliko ya katiba huku vyama vya upinzani vikipinga mpango huo na kueleza kuwa ni njama za rais Tshisekedi kutaka kuendelea kusalia madarakani.
