
Ijumaa, Machi 14, 2025
Kibondo, Kigoma
Madiwani Kibondo Wataka Serikali Kuboresha Mazingira ya Biashara
Madiwani kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma wameishauri serikali kuboresha vitegauchumi vyake ili kuwavutia wafanyabiashara wanaotaka kuwekeza na kukuza uchumi wa wilaya hiyo.
Akizungumza na Radio Kwizera, mmoja wa madiwani hao, Bw. Alex Baragomwa ambaye ni Diwani wa Kata ya Kibondo mjini, amesema kuna haja ya kuboresha maeneo mbalimbali, hasa masoko, ili kukuza uchumi wa Kibondo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Bw. Deokresi Lutema amesema serikali tayari ina mikakati endelevu ya kuboresha mazingira ya biashara ili kuvutia uwekezaji zaidi.